<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><title>Nilikuwa Kondoo Aliyepotea TZR30</title>
<lyrics>[V1]
 Nilikuwa kondoo aliyepotea,
 Sikupenda zizi kamwe, ila kutembea
 Nilikuwa mwana asiyesikia,
 Sikupenda baba yangu wala kutulia.

[V2]
 Na mchunga mwema alinitafuta,
 Baba kwa mapenzi ndiye aliyenivuta;
 Karibu ya kufa, kwa kiu na kwa njaa,
 Waliniona mnyonge, waliniokoa.

[V3]
 Yesu ni mchunga, mwenziwe hapana,
 Aliosha taka zangu, dhambi nyingi sana;
 Kwa vidonda vyangu alitia dawa.
 Ndiye aliyenipata, na kwake nalindwa.

[V4]
 Nilikuwa kondoo aliyepotea
 Sasa nampenda Baba, na mchunga pia;
 Kwanza nilitanga na kukosa sana,
 Hivi nyumbani mwa Baba sipotei tena.</lyrics>
<hymn_number>30</hymn_number>
</song>